AINA KUU ZA FASIHI NA TOFAUTI ZAKE
Fasihi simulizi ni istilahi inayotumiwa na kueleza dhana ya fasihi itolewayo kwa mdomo bila kuandikwa. Istilahi hii ilizuka miaka ya 1970. Fasihi simulizi ni sanaa inayotungwa au kubuniwa kwa kichwa na kuwasilishwa kwa mdomo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi simulizi ni tukio linalofungamana na muktadha fulani wa kijamii (Mulokozi 2017:37-38) Fasihi simulizi ni sanaa ya lugha inayotungwa na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Kuwapo kwa fasihi andishi hutegemea mambo matatu ambayo ni mtunzi (ambaye kwa kawaida ndiye mwandishi), hadhira (wasomaji) na mdhamini ambaye ni mchapishaji atakayeipigisha chapa kazi iliyoandikwa. Fasihi andishi imegawanyika katika kumbo mbili ambazo ni Nadhumu na Nathari. Nudhumu ni tungo za kishairi wakati nathari ni maandiko ya kimjazo yasiyofuata kanuni za kishairi. UHUSIANO WA FASIHI ANDISHI NA SIMULIZI Fasihi simulizi na andishi kuna mambo zinafanana, baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo a) Zote hutumia ufundi wa lugha il...