AINA KUU ZA FASIHI NA TOFAUTI ZAKE
Fasihi simulizi ni istilahi inayotumiwa na kueleza dhana ya fasihi itolewayo kwa mdomo bila kuandikwa. Istilahi hii ilizuka miaka ya 1970. Fasihi simulizi ni sanaa inayotungwa au kubuniwa kwa kichwa na kuwasilishwa kwa mdomo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi simulizi ni tukio linalofungamana na muktadha fulani wa kijamii (Mulokozi 2017:37-38)
Fasihi simulizi ni sanaa ya lugha inayotungwa na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Kuwapo kwa fasihi andishi hutegemea mambo matatu ambayo ni mtunzi (ambaye kwa kawaida ndiye mwandishi), hadhira (wasomaji) na mdhamini ambaye ni mchapishaji atakayeipigisha chapa kazi iliyoandikwa. Fasihi andishi imegawanyika katika kumbo mbili ambazo ni Nadhumu na Nathari. Nudhumu ni tungo za kishairi wakati nathari ni maandiko ya kimjazo yasiyofuata kanuni za kishairi.
UHUSIANO WA FASIHI ANDISHI NA SIMULIZI
Fasihi simulizi na andishi kuna mambo zinafanana, baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo
a) Zote hutumia ufundi wa lugha ili kuwasilisha ujumbe wake.
b) Zote hujadili dhamira zinazotokana na migogoro na matatizo ya mwanadamu katika mazingira yake.
c) Zote zina dhima zinazofanan kama vile kuelimisha, kuburudisha
d) Zina tanzu ambazo huzaliwa, hustawi na hufa kufuatana na wakati.
TOFAUTI YA FASIHI ANDISHI NA FASIHI SIMULIZI
a) Wahusika - fasihi simulizi hutumia wahusika ambao si binadamu kwa mfano wanyama, mimea na vitu visivyo na uhai. Fasihi andishi hutumia zaidi wahusika binadamu ni mara chache hutumia wahusika ambao si binadamu kama vile wanyama na mimea.
b) Umri - Fasihi simulizi ni ya kale zaidi. Fasihi andishi ni changa zaidi.
c) Utunzi - Fasihi simulizi hutumia muda mfupi kutungwa kwa vile huwa kichwani na husilishwa kwa kichwa pia. Fasihi andishi hutumia muda mwingi kutungwa kwa vile huhitaji kuandikwa na kuchapishwa mpaka ifike kwa hadhira.
d) Uwasilishaji - Fasihi simulizi huwasilishwa kwa mdomo ishara na vitendo. Fasihi andiahi huwasilishwa kwa maandishi.
e) Tanzu - fasihi simulizi ina tanzu nyingi zaidi. Fasihi andishi ina tanzu chache zaidi.
f) Uhifadhi - Fasihi simulizi huhifadhiwa kichwani wakati fasihi andishi huhifadhiwa kwa maandishi.
MUHTASARI
Katika makala hii umefahamishwa kuhusu
a) Aina kuu za fasihi ya kiswahili yaani fasihi andishi na fasihi simulizi
b) Uhusiano wa fasihi simulizi na fasihi andishi
c) Utofauti wa fasihi simulizi na andishi.
REJEA
Mulokozi, M.M (2017) Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili: Kozi za Vyuoni na Vyuo Vikuu.

ASANTENI
ReplyDeleteNimependa kazi Yako naomba msaada nifundshe namna ya kuzipata notes zako
ReplyDelete