UREJESHAJI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

UREJESHAJI KATIKA TUNGO ZA KISWAHILI
swali hili linatutaka kujadili ni kwa namna gani urejeshi unavyojitokeza katika tungo mbalimbali za lugha ya Kiswahili. Katika utangulizi tumeweza kutoa fasili mbalimbali kulingana na wataalamu tofautitofauti kisha kiini cha swali ambacho tumeonyesha ni kwa namna gani urejeshi unavyojitokeza katika baadhi ya tungo za lugha ya Kiswahili. katika hitimisho tukatoa majumuisho kuhusiana na mjadala wa swali. Tukianza na fasili za dhana mbalimbali katika swali kama ifuatavyo;-
TUKI (1990) wanaeleza kuwa urejeshi ni kitendo cha kuweka kiwakilishi ambacho huweza kutumiwa kupatanisha kishazi, kinachorejelea na kuvumisha kikundi nomino. yaani kishazi rejeshi kinafanya kazi ya kuvumisha nomino katika kikundi nomino hicho.
Massamba (2009) anaeleza kuwa kishazi rejeshi ni kishazi ambacho kina uamilifu wa kurejelea kwenye kirai nomino ambacho kinakibeba. Anafafanua kwamba kishazi bebwa ni kishazi ambacho hakiwezi kujitegemea chenyewe na ambacho kimechopekwa ndani ya kishazi kingine kikuu. kwa mfano
                              Hamida atakapowasili nitafurahi sana. katika sentensi hii kishazi kilichokozwa wino ndicho kishazi bebwa.

BAKITA (2013) Wanatumia istilahi urejezi na kuifasili kama ni uhusiano uliopo kati ya neno moja na jingine kwa kumrejesha msomaji kwenye neno au kidahizo cha msingi kilichokwisha tajwa au kitakachotajwa, kinachobainisha fasili ya neno husika.
Mekacha (1987) Anaeleza kuwa Tungo rejeshi ni aina mojawapo ya tungo tegemezi. Tungo tegemezi ni sentensi iliyoshushwa hadhi na kutegemezwa katika sentensi nyingine. Hii ni kusema kuwa tungo tegemezi haitokei peke yake; bali hutokea kama sehemu ya sentensi. kimuundo tungo tegemezi huwa kiambajengo ama cha sentensi kuu au cha kiambajengo kingine cha sentensi hiyo. kwa mfano,
Kuku aliyepotea jana amepatikana.
mwalimu amewaadhibu wanafunzi waliotoroka.
katika mifano hii tungo zilizokozwa ndizo tungo rejeshi.
Hivyo tunaweza kusema kuwa urejeshi ni kitendo kinachohusisha, upachikaji au kuchop,ekaji wa viambishi au vipashio vya maneno viinavyorejelea, aidha Nomino, Kiwakilishi au Kivumishi katika tungo za lugha ya Kiswahili. kuna viambishi tofautitofauti vinavyoonesha urejeshi katika lugha ya Kiswahili, ambavyo viambishi hivyo hujitokeza katika maumbo ya umoja na wingi ya ngeli za Kiswahili. kwa mujibu wa Samasoni ( 2016) anaonyesha jedwali la ngeli pamoja na viambishi vya urejeshi vinavyojitokeza.











Ngeli
Kirejeshi
                                   Mifano

i
A
-ye-
Mtoto aliyetoroka ameadhibiwa

ii
Wa
-o-
Watoto waliotoroka wameadhibiwa

iii
U
-o-
Mto uliofurika ni mara

iv
I
-yo-
Miti iliyokatwa imekauka

v
Li
-lo-
Jiwe lililotupwa limepotea

vi
Ya
-yo-
Meno yaliyong’oka ni ya mbele

vii
Ki
-cho-
Kijiko kilichopotea ni cha mezani

viii
Vi
-vyo-
Viti vilivyoletwa havitoshi

ix
I
-yo-
Nguo iliyonunuliwa inambana

x
Zi
-zo-
Nguo zilizochanika haziruhusiwi

xi
U
-o-
Ubao ulionunuliwa unatosha

xii
Zi
-zo-
Nyufa zilizozibwa zimetokea tena

xiii
U
-o-
Ugonjwa ulioenea hautabiriki

xvi
Ya
-yo-
Magonjwa yanayoambukizwa huzuilika

xv
Ku
-ko-
Kuimba kulikomfurahisha ni kwa Asha

xvi
Pa
-po-
Mahali paliposafishwa hapatoshi

xvii
Mu
-mo-
Chumba mlimoingia nyoka mna giza

Chanzo: Samsoni (2016)
hata hivyo swala la urejeshi katika tungo za Kiswahili halitokei kiholela tu bali kuna utaratibu maalumu. yaani muunganiko wa kishazi kimoja na kingine si wa kinasibu vilevile si kila kishazi kinaweza kuunganishwa na kishazi kingine;
Mekacha (keshatajwa) anafafanua baadhi ya masharti ambayo yanatawala katika kuunganisha vishazi pamoja na sentensi mbili au zaidi sahili. Ambapo sentensi moja au itakunjwa au zitakunjwa ndani ya sentensi nyingine, kwa mfano,
                                     Denis amevunja kikombe.
                                      kikombe kimepakwa rangi.
                                      rangi imenunuliwa Dubai.
Sentensi; Denis amevunja kikombe kilichopakwa rangi iliyonunuliwa Dubai.

Sharti jingine ni kwamba nomino zinazotajwa katika sentensi au vishazi. lazima ziwe zinarejelea kitu kilekile. kwa mfano;
Embe lililoiva limepote
Hivyo katika tungo hapo juu maneno yaliyokozwa yanarejelea neon embe.
Kirejeshi lazima kiwe karibu na kisabiki chake. kirai nomino cha kishazi bebwa lazima kiwe karibu na kirejelewa chake, kwa mfano
                                               Rabia amenunua daftari.
                                               Daftari ni zuri.
Itakua; Rabia amenunua daftari ambalo ni zuri. hivyo katika sentensi hii kishazi bebwa ni ambalo ni zuri. kinachojitokeza karibu na kisabiki chake ambacho ni daftari.
Sharti jingine la ukunjiaji wa kishazi au sentensi ni kwamba sentensi hizo zisiwe na ukanushi. hii inamaana kuwa sentensi kanushi haziwezi kugeuzwa kuwa urejeshi au kiambajengo cha sentensi nyingine. Kwamfano;
Watoto hawaruki Kamba.
Kamba hairukwi.
Steve ni mwerevu kuliko Juma.
Marwa ni mrefu kuliko Kapinga.
Katika tungo hapo juu urejeshi hauwezi kufanyika kwa sababu ya ukinzani na ukanushi, licha ya kuwa nomino zinarejelea kitu kile kile.
Kirejeshi huambishwa kwa namna tofautitofauti na namna hizo za uambishaji ndizo msingi wa uainishaji wa miundo mbalimbali ya tungo rejeshi nazo huitwa aina za urejeshi. Sifa kuu ambayo inatawala urejeshaji wa kila namna ni lazima kiwakilishi kifanane na kikundi nomino kinachokitawala. Sifa nyingine ni kwamba lazima kirejeshi kifuate mara tu baada ya kikundi nomino kinachorejewa; Urejeshi katika tungo za lugha ya Kiswahili, hujitokeza kwa namna tofautitofauti kama ifuatavyo;
Urejeshi katika lugha ya Kiswahili huweza kujitokeza katika umbo Amba ambalo huambikwa kiambishi cha urejeshi, mwishoni na kuwa na muundo wa AMBA + REJ
                                           a kitabu kilipotea.
                                           b kitabu kimeonekana.
sentensi; kitambu ambacho kilipotea kimeonekana.
                                         a Evo amepata adhabu.
                                         b Evo hawezi adhabu.
sentensi; Evo amepata adhabu ambayo haiwezi.
katika tungo hapo juu sentensi a na b ni sahihi ambazo zimeunganishwa kwa kwa kudunisha au kudhohofisha sentensi b na kuifanya kuwa kishazi rejeshi au tegemezi ambacho kinafanya  kazi kama kijenzi cha kirai nomino cha sentensi kuu. hivyo viambishi cho na yo ni viwakilishi virejeshi ambachokinarejelea kirai nomino cha sentensi kuu.
Kuchopeka kiambishi rejeshi baada ya kiambishi cha njeo. Hii ni namna mojawapo ya ujitokezaji wa urejeshi katika lugha ya Kiswahili kwenye tungo mbalimbali kulingana na mazingira fulani fulani ya tungo yenyewe. Katika namna hii viambishi vya urejeshi hupachikwa baada ya njeo ili kuonyesha urejeshi wa tungo hiyo mathalani katika lugha ya Kiswahili.
                                        Baba anakula chakula
                                        Baba anayekula chakula
                                        Mtoto alicheza mpira
                                       Mtoto aliyecheza mpira
                                       Moto utawaka
                                       Moto utakaowaka
Hivyo katika mifano hapo juu, tunaona kuwa maumbo kama ye na o ndiyo yamebeba urejeshi katika tungo hizo, na maumbo hayo ya urejeshi yamejitokeza baada ya maumbo ya njeo kama vile na, ta na li. Hivyo hii ni namna mojawapo ya ujitokezaji wa urejeshi katika tungo za lugha ya Kiswahili.
Urejeshaji pia hujitokeza kwa kupachika kiambishi cha urejeshi mwishoni mwa kitenzi na kudondosha kiambishi cha njeo. viambishi njeo ni viambishi ambavyo hudokeza muda wa t endo linapotokea, lililotokea, litakalotokea. Katika mazingira haya kiambishi cha urejeshi hupachikwa  baada ya mzizi au shina la kitenzi na umbo la njeo katika  kitenzi hudondoshwa;
kwa mfano
1a mafuta yanaponya
b mafuta yaponyayo

2a gari linauzwa.
b gari liuzwalo.
katika sentensi 1 na 2 hapo juu upachikwaji wa umbo rejeshi yo katika kitenzi cha sentensi ya kwanza na lo katika kitenzi cha sentensi ya pili, kumesababisha utegemezi wa tungo b katika              vimechopekwa baada ya viambishi njeo na hivyo kusababisha urejeshi kisha utegemezi katika tungo hizo.
urejeshi katika lugha ya Kiswahili hutegemea upatanisho wa kisarufi, yaani kuwe na uapatanisho wa kisarufi kati ya viambishi vya urejeshi na maumbo yanayorejelewa, kwa kuzingazitia njeo na maumbo ya umoja na wingi. Kwamfano; vifaa kilichopotea katika tungo hiyo kiambishi cha urejeshi cho kipo katika umbo la umoja lakini nomino inayorejelewa ipo katika umbo la wingi, Hivyo huonesha kuwa hakuna upatanisho wa kisarufi.Hivyo basi upatanisho wa kisarufi ni muhimu ili kuleta mantiki katika urejeshi wa tungo za Kiswahili.




MAREJELEO
BAKITA (2015) kamusi kuu ya Kiswahili. Longhorn Publishers.
Massamba D.P.B na wenzake (2009) Fonolojia ya Kiswahili sanifu: Sekondari na Vyuo. TUKI. Dar es salaam
Mekacha, R. (1987). Tungo Rejeshi katika Kiswahili katika Mulika Na. 10. Dar es Salaam: TUKI,
                      Uk. 83-91
Samson, E. (2016). Muundo wa Vishazi Tegemezi Bebwa katika Kiswahili. Tasnifu ya Umahiri.
                        Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
. Mekacha, 1987: 83 katika Mulika Na. 19;
TUKI (1990) Kamusi sanifu ya isimu na lugha. Dar es salaam: TUKI na Educational Publishers and Distributors Ltd.

Comments

Popular posts from this blog

AINA KUU ZA FASIHI NA TOFAUTI ZAKE

UKUMUSHI KATIKA VITENZI VYA KISWAHILI