UREJESHAJI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
UREJESHAJI KATIKA TUNGO ZA KISWAHILI swali hili linatutaka kujadili ni kwa namna gani urejeshi unavyojitokeza katika tungo mbalimbali za lugha ya Kiswahili. Katika utangulizi tumeweza kutoa fasili mbalimbali kulingana na wataalamu tofautitofauti kisha kiini cha swali ambacho tumeonyesha ni kwa namna gani urejeshi unavyojitokeza katika baadhi ya tungo za lugha ya Kiswahili. katika hitimisho tukatoa majumuisho kuhusiana na mjadala wa swali. Tukianza na fasili za dhana mbalimbali katika swali kama ifuatavyo;- TUKI (1990) wanaeleza kuwa urejeshi ni kitendo cha kuweka kiwakilishi ambacho huweza kutumiwa kupatanisha kishazi, kinachorejelea na kuvumisha kikundi nomino. yaani kishazi rejeshi kinafanya kazi ya kuvumisha nomino katika kikundi nomino hicho. Massamba (2009) anaeleza kuwa kishazi rejeshi ni kishazi ambacho kina uamilifu wa kurejelea kwenye kirai nomino ambacho kinakibeba. Anafafanua kwamba kishazi bebwa ni kishazi ambacho hakiwezi kujitegemea chenyewe na ambacho kimechopekwa nda...